Wednesday, 1 January 2020

UNAKIJUA KISA CHA LEYLA NA MAJNUN (mapenzi bikra)

Leyla na majnun ni kisa maarufu duniani kilichotokea kweli katika eneo la uarabuni... Na kwa kisa hiki kimepelekea kutungiwa mashairi mbali mbali duniani.... Wengine hukiita kisa hiki kama "Romeo na Juliette wa mashariki".....ni kisa chenye mafunzo kwa makubwa
Qays ibn al -Mullawah alipendana na bint mrembo aliyeitwa Layla al aamiriya...Qays mapenzi yalimzidia ikawa kila mara analitaja jina la mrembo Layla.... Ikafikia hatua anatunga mashairi ya kuonyesha mapenz yake kwa Layla, mashairi ya kuonyesha urembo wa layla, na kila muda haachi kulitaja jina la bibie layla
Yale mapenz yaliyomzidia hadi akashindwa kujitambua kwa mapenz yake kwa Layla hadi watu wa jamii yake walimuita Majnun (mwehu)
Qays alipeleka posa kwa ajili ya kumuoa Layla lakini baba ake na Layla alikataa posa ile akidai binti yake hawezi kuolewa na mtu mwehu
Na haikupita muda Layla akaolewa na Mwanaume mwengine... Mwenye hadhi ya juu na mfanyabiashara mkubwa na inasemekana alikuwa na mvuto mno (handsome) .....Uzuri wa mume wa Layla ulisababisha hadi ikawa anaitwa Uwaridi
Baada ya Majnun kusikia habari za ndoa ya Layla aliumia sana na kuamua kukimbia ule mji na kwenda jangwani.... Huko alilia sana huku akiimba mashairi ya mapenzi na mengine akiyaandika kwenye mchanga wa jangwani
Licha ya Familia ya Majnun kujitahidi kumpa Moyo ili arudi nyumbani lakini hawakufanikiwa
Baadae Layla na Mumewe waliamua kuhama mji na kwenda kaskazini mwa uarabuni ....huko aliumwa sana na kufariki.... Watu wengi wanasema kuwa kilichomuua Layla ni maumivu ya moyo kwa sababu baba yake amekataa kumuoza kwa mtu ampendaye (majnun)
Baada ya miaka kadhaa Majnun nae alikutwa amefariki pembeni mwa kaburi la Layla huku akiwa ameandika shairi lenye mistari mitatu kwenye mwamba uliokaribu na kaburi LA Layla
Shairi hilo limeandikwa kama ifuatavyo (shairi liliandikwa kwa kiarabu lakini hapa limetafsiriwa kwa Kingereza)
I pass by these walls, the walls of Layla
And I kiss this wall and that wall
It’s not Love of the walls that has enraptured my heart
But of the One who dwells within them ”
"Nimevuka Kati ya hizi kuta, kuta za Layla
Na nimezibusu kuta hizi
Sio mapenzi ya kuta ndio yalonipa furaha na amani katikaw moyo wangu
Bali ni huyu alive ndani ya hizi kuta "
Nb* tafsiri ya kiswahili sio rasmi ...nimeitafsiri tu mimi bwana fact

Qays na Layla wote walipendana... Tena mapenzi ya dhati lakini walikosa nguvu za kupigania penzi lao kwahiyo kila mmoja akabaki na maumivu yake moyoni ....Majnun Alichanganyikiwa kweli kweli na Layla hakupata furaha na amani ya ndoa
Walipendana lakini hawajawahi kuoana Waka kukutana kitanda kimoja na ndio maana yameitwa mapenzi bikra
umejifunza nini kupitia kisa hiki??

Image may contain: 1 person

Mama Maria Teresa akiwa na miaka 18

Image may contain: 1 person, smiling


Hapo ilikuwa ni mwaka 1928 katika mji wa Circa nchini Ireland....

Mama Maria Teresa alizaliwa mwaka 1910 katika mji wa Skopje nchini Macedonia

Tangu mdogo alitamani kuwa mtawa ili apate kuwasaidia masikini wenye uhitaji

Akiwa na miaka 18 alikubaliwa kujiunga na masista wa nchi ya Ireland

MALIKIA WA MWISHO WA MONGOLIA



Anaitwa Malikia Genepil alinyongwa mwaka 1938....kipindi ambacho wasoviet walikuwa wanaikalia kwa nguvu Mongolia
Katika kipindi hiko Kati ya mwaka 1937 hadi 1939 ambapo zaidi ya watu elfu 20 waliuwawa wakiwemo wana mapinduzi, mabhudhist, na watu wengine wengi
Image may contain: 1 person, indoor

ANDRE THE GIANT

bingwa wa kunywa bia duniani
Andre Rene Roussimoff ni mwanamiereka wa kfaransa na pia ni muigizaji
Amezaliwa mwaka 1946 na amefariki mwaka 1993
Huyu bwana anashikilia rekodi ya dunia kwa kunywa bia 119 ndani ya masaa sita tu..... Tunaweza kusema kila baada ya dakika 3 amekunywa bia moja bila kupumzika
Pia vyanzo vyengine vinasema amekunywa bia 153 bila kupumzika
Lakin mpaka sasa Hakuna mtu yoyote aliyefanikiwa kunywa bia nyingi kiasi hicho kwa wakati mmoja
Image may contain: 1 person, standing

Saturday, 28 December 2019

HOTEL KUBWA ZAIDI DUNIANI kufunguliwa 2020

Abraj Kudai ndio hotel itakayoshikilia rekodi ya ukubwa zaidi duniani pindi itakapoanza kutumika mwaka 2020

Hotel hiyo iliyotengenezwa katika mji wa maka nchi saudia arabia imegharimu Dolar za kimarekan Bilion 3.5 .....itakuwa na vyumba 10,000 na migahawa 70 na maduka makubwa ya bidhaa mbalimbali

Mji wa Maka una uhakika wa kupokea zaidi ya Mahujaji Milion 2 kila mwaka kwa ajili ya kufanya hija katika mji huo mtukufu wa waislamu

Lakini pia Mji wa Maka kwa mwaka mmoja unapokea zaidi ya Wageni Milion 20 ambao wanakwenda kwa ajili ya kutembea tu

Hotel hiyo itakuwa na vyumba vya kifahari kwa ajili ya watu matajiri, lakini pia kitakuwa na eneo maalumu kwa ajili ya familia ya kifalme ya nchi hiyo

Hotel hiyo imechukua eneo lenye ukubwa wa meter square 1,400,000

Itakuwa majengo marefu 12

Kwa sasa rekodi ya hotel kubwa inashikiliwa na hotel ya Genting Highland ya nchini Malaysia....hotel hiyo ina vyumba 7,351 kwa mchanganuo ufuatao

Standard rooms 3164

Deluxe rooms 2922

Triple deluxe rooms 649

Superior deluxe rooms 480

World club rooms 136

Ukijumlisha vyumba vyote hivi ndio unapata vyumba 7351 vya hotel hii inayoshikilia rekodi ya dunia kwa sasa....hadi hapo Abraj Kudai itakapofunguliwa

Image may contain: sky, cloud and outdoor

WANAUME NDIO WANAUMIA ZAIDI PINDI MAPENZI YANAPOVUNJIKA KULIKO WANAWAKE (ikiwa walikuwa wanapenda)

WANAUME NDIO WANAUMIA ZAIDI PINDI MAPENZI YANAPOVUNJIKA KULIKO WANAWAKE (ikiwa walikuwa wanapenda)
Wanasaikolojia wanasema kuwa pindi mahusiano ya kimapenzi yanapovunjika wanaume ndio wanaumia zaidi kuliko wanawake
Lakini kinachofanya jamii ione wanawake ndio wanaumia zaidi ni kutokana na kuww mwanaume hapendi kuonekana kuwa ameumia kwa ajili ya mapenzi hivyo hujikaza na kujionyeshe usoni kuwa hajaumia
Baada ya mapenz kuvunjika mwanaume huathirika zaidi na ni rahisi kwa mwanaume kujiingiza kwenye tabia zisizofaa pindi anapoumia kwa mapenz kuliko wanawake

VERONIKA SEIDER

.mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuona
Amezaliwa mwaka 1951 nchini ujerumani....na kwa sasa ni Daktar wa meno
Veronika ana uwezo wa kuona mara 20 zaidi ya binadamu wa kawaida
Veronika ana uwezo wa kuwatofautisha watu walio kwenye umbali wa zaidi ya maili moja ......yaan ni sawa na futi 5280
Visual acuity ya binadamu wa kawaida ni 20/20 ......
Lakini yeye ni 20/2